Rais John Magufuli amewawekea mipaka wawakilishi wa wananchi waliochaguliwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita, kuhakikisha wanafanya mikutano na maandamano kwenye maeneo yao bila kuingia kwenye eneo ambalo hawakuchaguliwa.

Akizungumza jana katika mfululizo wa ziara yake katika miji ya Singida, Tabora, Geita na Shinyanga akitokea mkoani Dodoma, Rais Magufuli alitoa mfano wa jimbo la Hai linaloongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe.

Rais alimruhusu Mbowe kufanya mikutano na maandamano ndani ya jimbo lake kadri awezavyo lakini ahakikishe havuki mpaka wa eneo hilo.

“Sio uliache jimbo lako la Hai uende Shinyanga ukawaambie waandamane wakati Hai hawataki kuandamana. Kawaandamanishe wa Hai hata usiku na mchana wawe wanaandamana, wanazunguka ili wakati tutakapokuwa tunavuna wao wanaandamana,” alisema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alipiga marufuku mpango wa Chadema kutaka kufanya mikutano na maandamano nchi nzima akisisitiza kuwa hatawavumilia. Aliwataka wasimjaribu kwani yeye ni tofauti na atakayetaka kumjaribu ‘atakiona’.

Kauli hizo za Mkuu wa nchi zimekuja saa chache baada ya Chadema kutangaza mpango wa kuzindua operesheni waliyoiita UKUTA (Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania), mpango uliolaaniwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Jaji Mutungi alisema kuwa tamko la Chadema lilijaa uchochezi na lugha zisizokubalika.

 

Mh. Possi Awataka Vijana Kuhakikisha Wanatumia Elimu Zao Kujiajiri
Daz Baba afunguka kuhusu dawa za kulevya, adai kukandamizwa na kutengwa