Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ametaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Seleman Jafo kumfukuza kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Geita kufuatia ubadhirifu wa fedha za halmashauri alioufanya.

Akizungumza jijini Dodoma baada ya kuapishwa Mawaziri na Manaibu Waziri, Rais Magufuli amemtaka Jafo kuanza na Mkurugenzi huyo aliyenunua gari la Shilingi Milioni 400 wakati bado halmmashauri hiyo ina uhitaji mkubwa katika sekta mbalimbali na huduma za jamii.

“Tamisemi kuna matumizi mabaya ya fedha, Jafo umefanya vizuri sana lakini kwenye kudhibiti fedha bado, nimefikiria sana kukurudisha au kutokukurudisha. Hapo nataka kusema ukweli tuelewane hili la matumizi mabaya. Unakuta mkurugenzi ananunua gari la milioni 400 fedha tumehangaika nazo kuzipata wananchi, watoto wanachangishwa unakuta madawati hayatoshi. Nataka  kazi yako ya kwanza kwenda kumsimamisha mkurugenzi wa Geita ndio kazi yako ya kwanza ukaanze nayo,” amesema Rais Magufuli.

Mwezi uliopita, Joseph Msukuma, Mbunge wa Geita vijijini alionekana katika mitandao ya kijamii akibainisha suala la Mkurugenzi wa Geita kununua gari lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 400 kinyume na makubaliano ya baraza la madiwani halmashauri na hii leo Rais Magufuli amesema gari hilo ni la gharama kuliko lile la Mkuu wa mkoa wa Geita.  

Tazama hapa chini kumuona Mbunge alivyoshindwa kuapa…

Magufuli asamehe wafungwa 3316, "Bora ninyongwe mimi"
Naibu Waziri ashindwa kuapa, JPM amtumbua hapohapo