Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, Kayombe Masoud Lyoba kutokana na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo wilayani humo.

Moja ya usimamizi mbovu ambao anadaiwa kufanya ni usimamizi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kwa kufanya ununuzi wa dawa ya mchwa kwa gharama kubwa ya milioni 66 kinyume cha gharama halisi.

Pia kutozingatia taratibu za manunuzi na miongozo ya matumizi ya fedha za ujenzi wa Hospitali za Halmashauri na kufanya ununuzi wa kokoto kwa gharama kubwa ya shilingi milioni 45 na kuzisafirisha kwa shilingi milioni 42.

Kutokana na utenguzi huo, Meneja wa TARURA Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Mhandisi Godfrey George Mlowe ndiye aliyeteuliwa kukaimu nafasi ya ukurugenzi wa Halmashauri hiyo.

Video: Walimu watakiwa kujiendeleza kimasomo
Waziri Kamwelwe aomba jengo la Terminal II likarabatiwe