Rais John Magufuli amemteua Jenerali mstaafu, George Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi ya Taifa (Tanapa).

Taarifa za uteuzi huo zimetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi ambaye ameeleza kuwa uteuzi huo umeanza jana.

Jenerali Waitara alikuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama tangu mwaka 2001 hadi mwaka 2007.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Eligy Shirika kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo. Uteuzi huo pia kwa mujibu wa Katibu Mkuu Kiongozi ulianza jana

Lowassa, Sumaye waweka mkakati mzito na wabunge wa Ukawa Dodoma
Exclusive: DJ D-Ommy Afunguka jinsi AY na Diamond walivyomsukuma kwenye jukwaa la kimataifa (Video)