Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli amemteua mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano.

Uteuzi huo umetangazwa Alhamis hii bungeni Dodoma na spika wa bunge, Job Ndugai aliyesoma barua iliyoandikwa kwa mkono na Dk Magufuli.

Kabla ya hapo, mheshimiwa Majaliwa alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Bunge limesimama kwa muda kupisha mchakato wa wabunge kuthibitisha uteuzi huo.

Mheshimiwa Majaliwa alizaliwa December 22, 1960.

Dk Tulia azungumzia taarifa zinazodai amepandikizwa Unaibu Spika
Wabunge wa Ukawa watishia Kufanya ‘Jambo’ Endapo Dkt Shein ataingia Bungeni na Dkt Magufuli