Rais John Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya TIB, Profesa William Lyakurwa.

Taarifa iliyotolewa na kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, imeeleza kuwa Rais Magufuli amechukua uamuzi huo kwa Mamlaka aliyonayo kisheria yaliyoanishwa katika kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria (Interpretation of Laws Act).

Kutokana na utenguzi huo, Rais amemteua Profesa Palamagamba Kabudi kuwa Mwenyekiti wa Benki hiyo kuanzia leo.

Mabadiliko hayo pia yamepelekea Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, kwa mujibu wa sheria ya tafsiri za sheria sura namba 1, kuivunja Bodi ya Wakurugenzi ya TIB na kuteua wajumbe wapya wa Bodi hiyo.

Wajumbe wapya walioteuliwa na Bodi hiyo ambao unaanza leo ni;

  1. Gen (Rtd) Mabula Mashauri
  2. Kazaki B. Lokina
  3. Rose Aiko
  4. Profesa Joseph Bwechweshaija
  5. Said Seif Mzee
  6. Arnold M. Kihaule
  7. Maduka Paul Kessy
  8. Charles Singili
''Team'' Zitumie Majina ya Wasanii Vizuri Siyo Kutukana Watu- Shilole
Exclusive: Jamal Kisongo Akanusha Uvumi Wa Mbwana Samatta Kuhamia Italia