Rais John Magufuli ametangaza kuiondoa mikataba yote ya mitambo ya kukodi ya ufuaji umeme chini ukiwemo mkataba wenye gharama kubwa ya kuuza umeme kati ya Tanesco kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Akiongea jana katika tukio la uzinduzi wa mradi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II utakaozalishwa Megawati 280, Rais Magufuli alimuagiza waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhakikisha kuwa nchi haiendelei na mikataba ya aina hiyo inayoligharimu taifa.

“Ni matumani yangu kuwa sitasikia tena mnaleta mapendekezo kwamba tunataka kuongeza mkataba huu au tunataka kukodi mtambo huu.Suala la kukodi likalegee, lizimie na life kabisa huko,” alisema Rais Magufuli.

Alisisitiza kuwa mawazo ya kukodi mitambo yanapaswa kufa na badala yake Tanzania inapaswa kuwa na uwezo wa kuzalisha umeme kwa kujenga mitambo yake.

Ripoti zinaonesha kuwa licha ya kuibuka sakala la Escrow lililoihusisha IPTL na baadhi ya mawaziri wa serikali ya awamu ya nne waliolazimika kujiuzulu kupitia Bunge la kumi, Tanesco imeendelea kuilipa IPTL shilingi bilioni 4.3 kwa mwezi kama ‘capacity charge’. Ingawa baadhi ya wabunge wameendelea kusisitiza kuwa ni bilioni 8 kwa mwezi.

“Tumechoka kuchezewa. Kuna miradi hapa ya hovyo kweli. Kila siku inazaa matatizo. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri (Muhongo) lisimamie hilo,” Rais Magufuli alikaririwa.

Aliwamwagia sifa Waziri Muhongo na Makonda kwa uchapakazi wao huku akieleza kuwa yeye hakuteua wanasiasa bali wachapakazi.

 

Magufuli na Mkewe wapiga simu ‘Live’ Clouds TV kama watazamaji wa kawaida
Ripoti: Tanzania yawa kati ya nchi 10 za mwisho kwa furaha duniani, fahamu sababu