Panga Pangua ya serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dk. John Magufuli inaendelea ambapo leo ametangaza kumteua Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Balozi Ombeni Sefue.

Taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Ikulu imeeleza kuhusu uteuzi huo mpya wa Katibu Mkuu Kiongozi na kueleza kuwa Balozi Ombeni Sefue sasa atapangiwa kazi nyingine.

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Kijazi alikuwa Balozi wa Tanzania nchini India.

Magufuli amemtumbua jibu Balozi Sefue kutokana na haya?
TCRA yadai 'Zigo Remix' ya AY imevunja Rekodi Ofisini Kwao, 'inapendwa'