Kasi ya Rais John Magufuli inayoenda sambamba na kubana matumizi imefanikisha kuokoa kiasi cha shilingi bilioni saba na milioni mia tano (7,500,000,000) zilizokuwa zikilipwa kwa watumishi hewa 7,795.

Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angellah Kairuki amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kingelipwa kama mishahara kwa watumishi hewa kuanzia Januari Mosi mwaka huu hadi Aprili.

Kugundulika kwa idadi hiyo ya wafanyakazi hewa kumefuatia agizo alilolitoa Rais John Magufuli mwezi uliopita kuwataka wakuu wa mikoa kwa kushirikiana na watendaji husika kuhakikisha wanawabaini watumishi hewa ndani ya wiki mbili.

Aidha, imebainika kuwa sekta ya Afya na Sekta ya Elimu ndizo zinazoongoza kwa kuwa na watumishi hewa.

Akiongea hivi karibuni Wilayani Chato mkoani Geita, Rais Magufuli alisema kuwa watumishi hewa wanatafuna fedha za umma na kwamba wamebaini kuwepo kwa mtumishi mmoja ambaye alikuwa akilipwa mishahara saba. Rais aliweka wazi kuwa Serikali imeamua kumfikisha mahakamani mtumishi huyo.

Mwana FA: Muziki wa Nigeria ni ‘Takataka’
Gardner Habash aleza faida/hasara baada ya kuachana na Lady Jay Dee