Uongozi wa kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBCR) kwa kushirikiana na Promota Jay Msangi umetuma ombi la kumtaka Rais Tanzania, John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi katika pambano la raundi 10 la uzani wa super welter kati ya Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay litakalofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Promota wa pambano hilo, Jay Msangi ameuweka hadharani mpango huo leo mchana alipozungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika studio za Azam TV jijini Dar es salaam, kwa kusema wanaamini ombi hilo litapokelewa.

“Tayari tumefanya taratibu zote za kumuomba rais wetu ambaye ni mpenzi wa michezo kuhudhuria pambano hilo,” alisema.

Awali Mwakinyo aliwahi kukaririwa akisema kwamba anajiandaa ili kushinda pambano hilo na ushindi wake utakuwa zawadi kwa rais Magufuli.

“Kitendo cha kunialika Ikulu na kunipa zawadi ya kiwanja mkoani Dodoma ilikuwa ni hamasa kubwa kwangu, lazima nishinde na ushindi wangu utakuwa zawadi kwa rais,” alisema Mwakinyo.

Southgate awashangaza England kwa kumuita kikosini Maddison
Video: ACT Wazalendo kukata rufaa wagombea wao kuenguliwa uchaguzi wa Serikali za mitaa

Comments

comments