Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli jana alisimulia moja kati ya sababu anazoamini zilimsaidia kushinda uchaguzi mkuu uliopita, uliokuwa na ushindani mkubwa kuwahi kushuhudiwa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.

Magufuli ameeleza kuwa zawadi ya kiroho aliyoipokea kutoka kwa Sister wa kanisa la Moyo wa Yesu mjini Singida iliyomfanya kushinda uchaguzi huo ndio sababu iliyompelekea kuamua yeye na mkewe kuhudhuria ibada ya Krismas katika kanisa hilo jana.

Alisema kabla hajaanza kampeni alipita katika kanisa hilo na kukutana na mtumishi huyo wa Mungu ambaye hamkumbuki jina. Mtumishi huyo alimpa rozari akimueleza kuwa itamsaidia kushinda uchaguzi. Rais Magufuli alieleza kuwa alizunguka na rozari hiyo katika kipindi chote cha uchaguzi.

“Hii ndio sababu kubwa iliyonifanya leo kuja hapa Singida kujumuika na wakaazi wake na Watanzania kwa ujumla kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo,” alisema Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli aliwataka wananchi kuacha kulalamika kuwa pesa imepotea na kwamba wasitegemee kuwa na pesa bila kufanya kazi.

Alisisitiza kuwa hata maandiko ya Mungu yanawataka watu kufanya kazi kwa bidii na kwamba asiyefanya kazi na asile.

Ridhiwani awapongeza watendaji Chalinze
Manara amuombea msamaha Jerry Muro