Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amesema serikali imeamua kusimamisha kwa muda usiozidi miezi miwili zoezi la utoaji ajira mpya na upandishaji wa vyeo kwa watumishi wa umma.

Amesema kuwa hatua hiyo inalenga kupisha uhakiki wa watumishi wa umma katika orodha ya malipo ya mshahara na kuondoa watumishi hewa.

Akizungumza wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya benki kuu ya Tanzania,amesema kuwa hatua hiyo hailengi kuwakatisha tamaa watumishi wa umaa.

pombee

Amesema kuwa shughuli za kuwaajiri na kuwapandisha vyeo maafisa hao itaendelea kama kawaida baada ya kukamilika kwa zoezi hilo.

“Serikali ninayoiongoza haina nia ya kuwakatisha tamaa wafanyakazi, lengo lake ni kujipanga kwa makosa tuliyoyafanya, na ndio maana nimesema kwa kipindi cha mwezi mmoja hivi au hata mwezi mmoja na nusu, haitazidi miezi miwili, tusiajiri mtumishi yeyote serikalini, lakini pia katika kipindi cha mwezi mmoja hatutawapandisha vyeo wafanyakazi.Ninaomba wafanyakazi waelewe hili, kwa sababu tukiendelea tutakuwa tunawapandisha vyeo hata wafanyakazi ambao hawapo, tunafanya ukaguzi wote tukishamaliza wafanyakazi wataendelea kupandishwa vyeo” alisema Rais Magufuli.

Wakati huo huo,Rais Magufuli ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania kuchukua hatua mara moja dhidi ya benki ambazo hazizalishi faida zikiwemo benki za serikali, kufuta akaunti mfu na kuanzisha mara moja akaunti moja ya mapato na matumizi ya serikali

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Magavana na Manaibu Gavana kutoka nchi 18 za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), Mabalozi kutoka nchi mbalimbali, Viongozi wa Taasisi za fedha za Afrika na Makatibu wakuu wa Wizara za Fedha na Mipango wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.

Akata Uume Wake Mkoani Tanga, Aamuriwa na Jini
Serikali Yaombwa Kufanya Marekebisho ya Sheria ya Mirathi