Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemshauri Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein kumuadhibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) kwa kugoma kumpa mkono hadharani.

Akihutubia umati mkubwa wa wananchi jana Kisiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya ziara yake visiwani humo, Rais Magufuli alionesha kushangazwa na moyo anaouonesha Dk. Shein kwa Maalim Seif hata baada ya kumfanyia kitendo hicho, huku akimshauri na yeye kugoma kusaini ruzuku za CUF.

“Mimi nisingeweza, niutoe mkono wangu hivi (anaonesha ishara) halafu uukatae… halafu kesho niende ofisini nijikunje kusaini kwa sababu ya matibabu yako !,” Rais Magufuli alisema.

“Ndio maana nasema wewe mzee Shein wewe ni special, nafikiri wanapotoka malaika wewe ndio unafuata.  Nikuombe mzee Shein, na jana nilizungumza. Kama mtu anaukataa mkono wako na wewe kata mkono wako kufanya mambo yake,” Alisema kwa msisitizo.

Aidha, Rais Magufuli alisisitiza kuwa hakutakuwa na uchaguzi wa marudio visiwani humo na kuwataka upande wa upinzani kutojihangaisha kuzunguka dunia ama wafuasi wao kufanya matendo ya uvunjifu wa amani kama kuchoma karafuu ili kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi wa marudio.

Mugabe; Nilikufa Halafu Nikafufuka
Mwakyembe; Serikali Imeimarisha Mahakama Zote Nchini Kuwashughulikia Wahalifu