Rais John Magufuli ametangaza vita kali na wafanyabiashara wasiozidi 10 ambao amesema ndio waliohodhi biashara ya sukari na kuua viwanda vya ndani.

Akizungumza hivi karibuni katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya PPF na NSSF mjini Arusha, Rais Magufuli alisema kuwa kati ya watu hao wamo ambao walihujumu kiwanda cha NMC na wanaposimama husema ‘CCM Oyee’.

“Wafanyabiashara hawa walinunua viwanda vya  NMC wakafungua mashine na kwenda kuuza Msumbuji na wakisimama utasikia ‘CCM Oyee’,” alisema Rais Magufuli.

Alisema kuwa atapambana na watu hao bila kujali ni wafuasi wa chama gani cha siasa.

“Utakuta watanzania wanaendeswa na wafanyabiashara  kati ya watano au kumu tu, ukienda kwenye suakari ni haohao, waliouwa viwanda ni haohao, nawahakikishia nitalala nao mbele hadi mwisho,” Rais Magufuli anakaririwa na gazeti la Mwananchi.

Alisema kuwa anafahamu kuna watu ambao wanajaribu kumkwamisha katika jitihada zake lakini atawashinda.

Thomas Vermaelen Kusaidia Mipango Ya Kutetea Taji
Chris Coleman Amtema Gareth Bale

Comments

comments