Rais John Magufuli ametoa siku saba kwa wafanyabiashara wanaomiliki makontena yaliyopotea bandarini na kukwepa kulipa kodi, kujisalimisha na kulipa kodi.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam alipofanya mkutano na wafanyabiashara na wadau wa sekta binafsi.

“Ninatoa siku saba, kuanzia leo, wafanyabishara hao wajisalimishe walipe kodi. Baada ya siku saba basi sheria itafuata mkondo,” alisema rais Magufuli. “Sisi tunachotaka ni kodi yetu tu,” alisisitiza.

Magufuli na Wafanyabiashara

Katika hatua nyingine, rais Magufuli aliwataka wadau wa sekta binafsi kuendelea kushirikiana na serikali katika kujenga uchumi wa nchi kwa kuwa sekta binafsi na serikali zinategemeana.

Magufuli Atoa Siri Ya Kwanini Anaweza ‘Kutumbua Majipu’ Bila Kujali Jina
Waziri Mkuu Ashtukiza Tena Bandarini, Akuta Madudu Mengine