Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli amesema kuwa tayari amekwishajihakikishia ushindi wa kishindo wa asilimia 80 na kwamba yeye ndiye rais ajaye wa Tanzania.

Dk. Magufuli ametoa kauli hizo jana katika mikutano ya kampeni aliyoifanya Mkoani Arusha ambapo alieleza kuwa hivi sasa anaendelea kuzunguka kwa lengo la kuongeza kiwango cha ushindi wake.

Aliwataka wananchi kutopoteza muda wao kumpigia kura mgombea mwingine kwa kuwa yeye ndiye mshindi na anasubiri kuapishwa kuwa rais wa serikali ya awamu ya nne baada ya zoezi la kupiga na kuhesabu kura, Oktoba 25.

Aidha, Mgombea huyo ambaye alipata mapokezi makubwa Mkoani humo ikiwa ni pamoja na umati mkubwa uliohudhuria katika kampeni zake kwenye jimbo la Monduli ambalo ni ngome ya mpinzani wake Edward Lowassa, aliwaahidi wananchi wa Arusha kuwa atawaletea maendeleo makubwa na kulifanya jiji la Arusha kuwa jiji la Kimataifa.

Alieleza kuwa jiji hilo linadumaa kimaendeleo kutokana na harakati za maandamano ya mara kwa mara.

Akiwa Monduli, Dk. Magufuli aliwataka wananchi hao kumpigia kura nyingi ili kwa kuwa ndiye atakayeondoa kero zao, huku akisifia juhudi zilizofanywa na mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Marehemu Edward Sokoine na kuahidi kumuenzi.

Dk. Magufuli pia alimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Namelock Sokoine ambaye alilelewa kisiasa na mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

 

Kumbe Liverpool Hawakua Na Lengo Na Klopp!!
Lukas Josef Podolski Aondoka Kambini