Wakurugenzi wawili wa halmashauri za Kigoma Ujiji, pamoja na Pangani wamesimamishwa kazi kuanzia leo na Rais Magufuli baada ya manispaa zao kukutwa na hati chafu baada ya kufanyiwa ukaguzi.

Rais Magufuli ametengua nafasi hizo leo wakati akipokea ripoti kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali, Profesa Musa Assad ambapo ripoti hiyo imeonyesha manispaa hizo kuwa na hati chafu.

Amesema kwamba ameamua kuchukua hatua hizo kwa sababu wameaibisha serikali na anaamini kupitia  wakurugenzi hao litakuwa fundisho kwa wengine.

“Kuna Wilaya mbili, Halmashauri Mbili zina hati chafu, Mimi nafikiri Kigoma Ujiji na Pangani, Mimi nafikiri saa nyingine tuchukue hatua kwa vile Waziri wa TAMISEMI upo hapa WAKURUGENZI wa Wilaya hizo WASIMAMISHWE kazi leo” -Rais Magufuli.

Mh. Rais amesema kuwa siyo vizuri sana kufanya utenguzi lakini lazima hatua zichukuliwe kwani hata wenyeviti wa kamati za bunge wamemshauri kuchukua hatua kwani   amesema kama hatua kama hizo zisipochukuliwa hatutafika mbali.

 

Nondo asimamishwa masomo UDSM
Joachim Low: Tunaiheshumu Brazil