Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewaasa Viongozi wa Mkoa wa Tabora kuacha majungu kutokana na eneo hilo kutawaliwa na majungu baina ya viongozi na viongozi pamoja na wananchi.

Rais Magufuli ametoa rai hiyo leo Januari 30, wakati akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Tabora katika viwanja vya Ali Hassan Mwinyi ambapo amewataka viongozi mkoani humo kuzungumza huku akiwaeleza wazi viongozi pamoja na wananchi kuwa kuwa majungu hayajengi na wala hayaleti maendeleo.

“Tuijenge Tabora kwa kuwa na umoja, tatizo moja ninaloliona hapa Tabora ni majungu, ukigeuka huku kuna jungu, huku unakutana na jungu, majungu hayajengi Mkoa, Viongozi wa Chama na Viongozi wa Serikali mliopepwa mamlaka Tabora jengeni umoja sio majungu” amesema Rais Magufuli.

“Mbunge wa hapa Tabora anapigwa vita wakati katika Wabunge wote Mwenyekiti wa Maadili ni huyu lakini anapigwa vita, hatuwezi kuwa wote Wabunge, mumtake au hamumtaki ataendelea kuwa Mbunge, Viongozi wa Dini iombeeni Tabora majungu yapungue” ameongeza Rais Magufuli.

“Kila mmoja hapa Tabora anapigwa majungu, RC unapigwa majungu, DC unapigwa majungu, Mkuu Wa Mkoa naamini utaitisha kikao mumalize majungu yenu hapa, nimechoka kusikia majungu, tunataka maendeleo ya Tabora sio majungu, sehemu yenye majungu huwa haiendelei”

Aidha Rais Magufuli ameeleza jinsi ambavyo majungu miongoni mwa wanachi mkoani humo yaliathiri idadi ya wananchi walioshiriki zoezi la kupika kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020.

“Baba wa Taifa amesomea hapa Tabora, Ukombozi wa Taifa umeanzia hapa, iweje hapa pawe kitovu cha kupika majungu, hata Wabunge na Madiwani mnapigana majungu chinichini, haya majungu Tabora yamefanya hata waliopiga kura wawe wachache, wamepiga 37% tu” amesema Rais Magufuli.

 

Waziri Jafo atangaza wiki ya kujifukiza
UN yatangaza udhibiti wa uuzaji chanjo