Viongozi walioteuliwa na Rais, John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, wakiwepo wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi pamoja na viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama wamepewa mtihani mzito endapo wataenda kugombea kwenye majimbo kwani watakuwa hawajaridhika na nafasi walizopewa.

Akitolea mfano kwa IGP Simon Sirro, amesema ” Nitamshangaa sana IGP kama ataondoka hapa aende akagombee bunda, akaombe ubunge akitegemea nitamteua kuwa Waziri (akicheka)….kwanza hana uhakika kama atashinda kura za maoni, na inawezekana akashinda bado nikamfuta”

Ameongeza kuwa kama angemtaka awe Waziri angemteua kwenye nafasi ya wabunge wa kuteuliwa na kumpa uwaziri, hivyo akienda kugombea itategemea siku ya kukata majina ameamkaje kwani anaweza kumfuta.

Aidha amewataka viongozi wateule kujitahidi kuelewa historia ya chama chao kilivyo kwani demokrasia ipo huru lakini wanatakiwa kulidhika na madaraka kwa kila mahali nafasi waliyonayo wanaweza kufanya maajabu kwani hawawezi kupata kilakitu.

Wabunge watunga sheria kumpa nguvu zaidi Rais – Rwanda
Watoto na tiketi feki wavuruga kampeni ya Trump