Rais John Magufuli amewapa saa takribani nne mawaziri wote ambao hawakujaza Tamko la rasilimali, maslahi na madeni pamoja na uadilifu, kujaza fomu hizo na kuziwasilisha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma vinginevyo watakuwa wamejiondoa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametangaza agizo hilo la Rais Magufuli, leo mchana alipofanya mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

“Mheshimiwa Rais ameelekeza mawaziri ambao hawajakuza tamko la rasilmali au hati ya ahadi ya uadilifu wafanye hivyo na kuzirejesha kabla saa 12 jioni,” alisema Waziri Mkuu. “Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake,” aliongeza.

Aliwataja Mawaziri hao waliokiuka sheria ya maadili ya utumishi wa umma kwa kutojaza fomu hizo na kurejeshwa kuwani Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga,  Waziri wa Nchi ( Muungano na Mazingira), January Makamba, Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, pamoja na Naibu Waziri wa  Nchi (Muungano na Mazingira), Bw. Luhaga Mpina.

Agizo hilo la Rais Magufuli limekuja ikiwa ni siku moja baada ya  Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Kaganda kudhihirisha kuwa wapo mawaziri ambao wamegoma kuwasilisha hati hizo za kiapo na kwamba majina yao yangewasilishwa kwa Waziri Mkuu kwa ajili ya hatua sitahiki.

Jaji Kaganda aliyasema hayo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya siku moja kwa mawaziri na Naibu mawaziri kuhusu sheria ya maadili, mgongano wa maslahi na mwongozo maadili ya vionzogozi wa umma na utekelezaji wa ahadi ya uadilifu.

Arsenal Kumkosa Chamberlain Kwa majuma Kadhaa
Sunday Oliseh Aachia Ngazi Nigeria