Rais John Magufuli ameridhia mawaziri wawili wa Serikali yake kufanya ziara nje ya nchi ikiwa ni miezi minne tangu alipoingia madarakani na kuweka zuio la safari za nje zisizoidhinishwa na Ikulu.

Tangu aingie madarakani, kati ya mawaziri wake, ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pekee waliwahi kutoka nje ya nchi.

Rais Magufuli jana aliwaruhusu Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba kwenda nchini Vietnam kwa lengo la kujifunza mbinu za  maendeleo baada ya kuvutiwa na kasi ya maendeleo ya muda mfupi ya nchi hiyo.

Uamuzi huo wa Rais Magufuli umekuja siku moja baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Vietnam, Truong Tang Sang aliyeitembelea Tanzania.

“Kutokana na hatua waliyopiga, Rais ameniruhusu mimi na Waziri wa Kilimo, Mwigulu Nchemba kwenda nchini humo muda mfupi baada ya Rais Truong kuondoka,” alisema Mwijage muda mfupi baada ya kumtembeza Rais wa Vietnam kwenye eneo Maalum la Uwekezaji la Benjamini Mkapa (EPZ) lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.

Simba Yasikitishwa Na Taarifa Za Abel Dhaira
Allan Wanga: Nitawafunga Bidvest Wits