Rais John Magufuli amewataka viongozi wa Chama Cha Wananchi (CUF), kuacha kuota ndoto za mchana kuhusu kufanyika kwa uchaguzi mwingine visiwani humo kabla ya mwaka 2020.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Pemba katika sehemu ya ziara yake visiwani humo.

“Uchaguzi mkuu umekwisha, na uchaguzi Mkuu mwingine Zanzibar ni hadi mwaka 2020. Huu ndio ukweli na hakuna kitakachoubadilisha,” alisema Rais Magufuli.

Kauli hiyo ya Rais Magufuli imekuja mwezi mmoja baada ya Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea urais wa chama hicho katika uchaguzi wa Oktoba 25 uliofutwa, kuzulu mataifa ya Magharibi akijaribu kuyashawishi kuibana Serikali ya CCM kwa madai kuwa ilipora ushindi wa chama hicho.

Maalim Seif amekuwa akisisitiza kuwa yeye ndiye aliyeshinda katika uchaguzi mkuu uliopita huku akidai kuwa chama hicho kitaendelea kutoitambua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hadi itakapojiondoa na kuitisha uchaguzi mwingine.

Rais Magufuli alisema kuwa Dk. Ali Mohamed Shein ndiye Rais halali wa Zanzibar.

NHC kupiga mnada mali za Mbowe
Rais Magufuli ataka Jecha apewe Tuzo ya heshima