Agizo la rais John Magufuli kuelekeza zaidi ya milioni 200 zilizokuwa zimechangwa kwa ajili ya sherehe ya kupungua Bunge la 11 kutumika kununua vitanda katika hospitali ya Muhimbili limewezesha kuwatoa sakafuni zaidi ya wagonjwa 300.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema kuwa fedha hizo zimewezesha kununua vitanda 300 vya wagonjwa pamoja na magodolo yake, shuka 600 na baiskeli za wagonjwa pamoja na vifaa vingine. Aliongeza kuwa vitanda hivyo tayari vimewasilishwa kwa uongozi wa hospitali hiyo na kwamba vitaanza kutumika leo.

Wadau mbalimbali walichangia zaidi ya milioni 225, kwa ajili ya sherehe hiyo lakini Rais Magufuli aliagiza zitumike kati ya milioni 10 hadi 20 na kiasi kinachobaki kitumike kununua vitanda na magodolo kwa ajili ya wagonjwa katika hospitali ya Muhimbili.

Polisi wanasa dawa za kulevya Uwanja wa Ndege
Sheria mpya ya Usalama Bararani kuwanyoosha madereva 'kielekroniki'