Rais John Magufuli amewazungumzia waliokuwa vinara katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadae kuhamia vyama vya upinzani katika uchaguzi wa mwaka jana.

Akizungumza jana na viongozi wa ngazi za Mkoa na Wilaya wa CCM, Dk. Magufuli aliwataka kuweka kando tofauti zao zilizotokana na vuguvugu la uchaguzi uliopita akiwataka wagange yajayo.

Dk. Magufuli anayetarajia kuwa Mwenyekiti wa CCM hivi karibuni alieleza kuwa huenda  waliokihama chama hicho mwaka jana ndio waliosababisha akashinda uchaguzi.

“Lakini inawezekana wale walifanya uamuzi wa kwenda kule walinisaidia mimi kushinda,” alisema Rais Magufuli bila kufafanua wala kuwataja majina.

Baada ya mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwaka jana, Mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye walitangaza kuihama CCM na kuhamia upande wa upinzani.

Lowassa alipewa nafasi ya kugombea urais kupitia Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, baada ya jina lake kukatwa na Kamati ya Nidhamu na Usalama kulikata jina lake.

Vinara wengine wa CCM waliohama ni pamoja na mwanasiasa mkongwe, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru aliyekuwa na kadi namba 8 ya chama hicho. Ingawa hakujiunga na chama kingine cha siasa, alimnadi mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Baadhi ya wenyeviti wa ngazi mbalimbali wa CCM, madiwani na wabunge walihamia upinzani.

Nape awafungukia wapinzani baada ya kususia Bunge
Ofisi ya Waziri Mkuu kutumia Bodaboda, Bajaji kubana matumizi