Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Magufuli amesema kuwa hakuna mtu ambaye alimkopesha fedha kwa ajili ya kuwapa rushwa wapiga kura ili wamuunge mkoni, hivyo hana deni la kurudisha.

Dkt. Magufuli aliyasema hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi katika viwanya vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, ambapo alidai kuwa katika kampeni yake hajawahi kumpa mtu rushwa ili amuunge mkono.

“Kama kuna mtu niliyempa rushwa kwenye kampeni zangu na yuko hapa anyooshe mkono,” aliuliza na kushangiliwa na watu waliohudhuria mkutano.

Alijinadi kuwa msafi na muadilifu katika kipindi chote alichokuwa akifanya kazi katika nafasi mbalimbali katika serikali ya awamu ya tatu na awamu ya nne.

“Kama ningekuwa mla rushwa ningekuwa bilionea. Miaka 20 nimekuwa nafanya kazi kwenye wizara tofautitofauti, nimesimamia miradi inayogharimu mabilioni ya pesa,” aliongeza.

Mgombea huyo alieleza kuwa amekuwa akifanya kazi ya kuunganisha Tanzania kwa barabara na kazi hiyo inaendelea, na hivi sasa wanafanya jitihada zote kupunguza msongamano wa magari kwenye majiji makubwa.

 

 

 

 

Chadema wataja asilimia za ‘ushindi wa Lowassa’
Eden Hazard Atikisa Kibiriti Chelsea