Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ameipongeza  Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kwa kupandishwa hadhi na kuwa jiji na kusema kuwa Halmashauri hiyo inastahili kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwani hata kwa mujibu wa ripoti wanaongoza katika mapato.

Rais Magufuli amesema hayo leo Februari 25, 2021 wakati akizungumza na Wananchi katika viwanja vya Mnazi mmoja jiji Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Mstahiki Meya wa iliyokuwa Manispaa ya Ilala pamoja na Naibu Meya wanastahili kuwa Mameya wa Jiji hilo.

“Nawapongeza sana Watu wa Ilala kwa Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es salaam, hongereni sana, mnastahili wala hamkupendelewa, hata kwenye taarifa iliyotolewa na Waziri inaonekana mnaongoza kwa mapato, sasa kwa nini mlinganishwe na Manispaa Manispaa!?” amesema Rais Magufuli.

“Meya wa Ilala na Naibu wako nyinyi ndio Maboss wa Jiji la Dar, na nyinyi Madiwani ndio Madiwani wa Jiji, baadhi ya Barabara ni mbovu kwa sababu mlikuwa mnalinganishwa mapato na Manispaa nyingine sasa bajeti yenu itakuwa kubwa hamuwezi kulinganishwa na Kino, Kigamboni au Temeke,” ameongeza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewataka watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuwa waaminifu katika kazi zao na wajifunze kutoa haki kwa wafanyabishara ambao wana nia ya kulipa kodi huku akiitaka Wizara ya Fedha kusimamia suala hilo kwa kuwa nchi inahitaji kodi pamoja naushuru ulio wa haki.

Rais Magufuli ametoa wito huo kufuatia uwepo wa baadhi ya watumishi ambao huwakadiria wafanyabishara kodi kubwa na wanaposhindwa kulipa huwataka  kugawana kile kiasi kidogo ambacho mfanyabiashara anakuwa nacho.

Senzo aijibu Simba SC
Young Africans yaiandalia 'DOZI' Kengold