Warizi wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli ambaye pia ni mgombea urais kwa tiketi ya CCM amewaahidi wananchi kuwa endapo watamchagua kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atakuwa rais asiye na majivuno anaewatumikia watu.

Magufuli ametoa ahadi hiyo jana alipokuwa akiwahutubia wanachama wa CCM katika makao makuu ya chama hicho Mkoani Mtwara.

“Nataka niahidi kwenu, na nimuombea Mungu na naomba dua zenu, nitapenda niwe mtumishi wa watu. Nisiwe na majivuno, nisijione, niwe mtumishi wa watu hasa wanyonge. Niweze kuwatumikia na kutimiza matarajio yao. Matarajio ya watanzania ni makubwa na matarajio ya wana Mtwara ni makubwa,” alisema Dk. Magufuli.

Mgombea huyo wa urais kupitia CCM alifanya ziara yake mkoani Mtwara ambapo aliambatana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Katika ziara hiyo, Magufuli alikagua miradi mbalimbali na kuzindua kivuko cha MV Mafanikio kinachofanya safari zake kati ya Mtwara Mjini na Mtwara Vijijini.

Lowassa Awavuta Boda Boda, Machinga Na Mama Ntilie
Yaya Toure Auwasha Moto Man City