Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amewataka wananchi kumchagua kwa kipindi kingine cha miaka mitano ili wampime baada ya miaka 10.

Dkt. Magufuli ambaye ni Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano akiwania urais kwa muhula wa pili, ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa Kampeni uliofanyika katika viwanja vya Kambarage Mjini Shinyanga.

Ameeleza miradi ambayo Serikali yake itatekeleza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo endapo atachaguliwa tena, ikiwa ni pamoja na miundombinu ya reli ya kisasa na usafirishaji.

Mgombea huyo wa urais amesema kuwa Serikali yake itajenga reli ya kisasa (SGR) yenye thamani ya Sh. 3 trilioni, itakayounganisha Isaka – Shinyanga hadi Mwanza, mradi ambao amesema utaanza kujengwa hivi karibuni.

Reli hii ya kisasa itaungana na mradi wa SGR ulioanzia Dar es Salaam hadi Makutupola jijini Dodoma.

“Jamani reli hii ya kisasa ni kama zile ambazo zinaonekana Ulaya… tumefanya mengi na tutaendelea kufanya makubwa tukiingia tena madarakani,” amesema Magufuli.

Amesema kuwa atatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya chama chake ambayo imeahidi kujenga viwanja vingine vya ndege, kununua ndege nyingine ikiwa ni Pamoja na ndege ya mizigo itakayosafirisha nyama na bidhaa nyingine kutoka nchini kwenda Ulaya.

Kampuni ya Total yawajibu wanaodai inaondoka Tanzania
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 4, 2020