Mgombea urais kupitia CCM, Dkt. John Magufuli ameendelea kufanya kampeni zake katika kipindi hiki cha lala salama ambapo jana alikuwa Mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo alitumia nafasi hiyo kuonesha masikitiko yake kwa mgombea urais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein kutokana na kauli za mpinzani wake, Maalim Seif Sharif Hamad (CUF).

Dkt. Magufuli alieleza hayo alipokuwa akiuhutumia umati mkubwa uliohudhuria mkutano huo.

“Nakuhurumia sana Dkt. Shein, umefanya kazi ngumu. Unaleta maendeleo kwa wananchi makamu wako anasimama hadharani anasema serikali haikufanya chochote, wananchi mtemeni huyo,” alisema.

Aliwataka wananchi kumpigia kura za ndiyo Dkt. Shein ili aendelee kuwa rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na yeye kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili waweze kuwaletea maendeleo ya kweli kwa usawa kati ya pande zote mbili.

Aidha, alisema kuwa serikali yake itahakikisha inapambana kikamilifu na maharamia wa kigeni wanaofanya uvuvi haramu katika eneo la bahari ya Hindi liliko nchini.

Dkt. Magufuli pia aliahidi kushirikana na mgombea mwenza, Samia Suluhu kuhakikisha anamaliza kero za Muungano alizodai zilikuwa 17 na sasa zimebaki kero 3 tu.

Naye Dkt. Shein alimhakikishia Dkt. Magufuli kuwa lazima atakuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba wagombea wengine wanamsindikiza kuingia ikulu.

Arsene Wenger Aahidi Neema Kabla Hajaondoka
Lowassa Amemkwepa Magufuli..?