Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa hawapi ahadi za uongo kwakuwa anataka kwenda mbinguni.

Akizungumza jana kwenye mkutano wa kampeni katika eneo la Misigiri mkoani Singida akiomba kura kwa wananchi, Magufuli amesema kuwa anataka afanye mambo mazuri duniani ili atakapofika mbinguni apewe nafasi nyingine ya kuwaongoza Malaika.

“Mimi sitoi ahadi za uongo kwa sababu msema kweli ni mpenzi wa Mungu, sitaki nifanye dhambi kwa kuwaambia wazee wangu uongo, ninapenda na mimi siku moja nifike mbinguni ili nikifika Malaika waniambie ulifanya vizuri tunakupa sasa hata ka Uwaziri wa Malaika,” amesema.

Katika hatua nyingine, mgombea huyo wa urais aliwaombea kura wagombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, Dkt. Mwigulu Nchemba na Profesa Kitila Mkumbo.

“Mwigulu ninamfahamu na ninampenda sana, lakini Mwigulu ni kama mdogo wangu maana amesoma Chuo Kikuu na mdogo wangu na Profesa Mkumbo ni mdogo wangu naye nampenda sana, ndiyo maana nikasema huyu agombee hapa na yule akagombee Ubungo na watashinda na mimi najua nitafanya nini,” alieleza.

Mgombea huyo amefanya kampeni katika Mkoa wa Singida ikiwa ni sehemu ya ratiba ya kampeni iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Wagombea wengine pia wameendelea kuomba kura, kila mmoja akiwaahidi makubwa Watanzania ili wampigie kura za ushindi Oktoba mwaka huu.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 3, 2020

Waziri mkuu kuunda serikali ndani ya wiki mbili – Lebanon

Membe: Tutakuwa mishumaa, haibiwi mtu, ni kivumbi
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 3, 2020