Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameapa kukomesha urasimu na kupambana na rushwa serikalini endapo atachaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiongea katika mkutano wa kampeni jana Babati Mjini, Dk. Magufuli alisema kuwa serikali yake itakuwa na watu wachapa kazi na itaondoa utaratibu wa watendaji kuwazungusha wananchi pindi wanapotaka huduma mbalimbali za kiserikali. Alisisitiza kuwa serikali yake itafuta usumbufu wa ‘njoo kesho’ katika ofisi za serikali.

“Nipeni urais muone nitakavyofunga mianya ya rushwa na ushuru usio maana. Mwananchi akiwa na nyanya zake ushuru, ukienda kuuza vitumbua ushuru, ukiwa na kambuzi kako unapeleka mnadani ushuru, mimi John Magufuli nataka kwena kufuta viushuru ushuru kama hivyo,” Dk. Magufuli alisema.

Magufuli Babati

Aliwataka wananchi wamuamini kwa kuwa anataka kuwaletea maendeleo ya kweli na atafanya kazi kwa ajili ya wananchi wote bila kujali vyama vyao vya siasa, huku akiwataka wasikubali kudanganywa na wagombea wengine kwa kuwa yeye ndiye anayefaa zaidi kuwaletea maendeleo.

Samatta Atimiza Wajubu Wake TP Mazembe
Lowassa Ampa Mkono Kingunge, Atangaza Neema Kwa Wenyeviti Serikali Za Mtaa