Nyanza, Kenya. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, John Pombe Magufuli na Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama wanatarajiwa kuwasili nchini Kenya siku tofauti mkoani Nyanza.

Rais Magufuli ataungana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga katika ziara maalum itakayofanyika kusini mwa Nyanza Ijumaa ya wiki ijayo.

Siku kumi baadaye Obama atafika kaunti ya Siaya mahali ambapo alizaliwa baba yake mzazi.

Odinga aliandaa mkutano na viongozi wa Nyanza akiwa na Gavana wa Migori Okoh Obado kupanga ujio wa viongozi hao.

”Nilikutana na viongozi hao na watakavyopokelewa na viongozi husika” amesema Odinga.

Hata hivyo Odinga hakutaka kueleza zaidi ujio wa viongozi hao na uhusiano wa karibu unaofanywa na upinzani kwa kushirikiana na Serikali iliyopo madarakani.

Pia Obama anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kituo cha michezo na ufundi kijulikanacho kwa jina la Sauti kuu kilichoanzishwa na dada yake Dk Auma Obama.

Askofu mwenye watoto 149 afungwa, ana wake 24
Rwanda yazindua gari la Volkswagen

Comments

comments