Rais Dkt. John Magufuli amesema anapoteua viongozi mbalimbali hapa nchini haangalii undugu, bali utendaji wao wa kazi kwenye nafasi za awali ambazo walikuwa wanasimamia.

Ameyasema hayo wakati akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma na kutolea mfano wa Dkt. Allan Kijazi kuwa hajachaguliwa kwasababu ya undugu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

“Nahili nataka niweke wazi undugu ni pembeni. Sio kwamba nimempa vyeo viwili lakini najua atakapokuwa anafanya Unaibu Katibu Mkuu na TANAPA pia akaisimamie ilikusudi tupate production nzuri.” amesema Rais Magufuli

Na kusisitiza “Kijazi amefanya kazi vizuri akiwa mtendaji wa TANAPA kwa miaka mingi ameweka rekodi yake vizuri na ndiyo maana nikasema kwa sababu imepatikana furusa kwenye wizara hii akawe Naibu Katibu Mkuu lakini ataendelea pia kufanya kazi za TANAPA ni kwa sababu sikupata wa kureplace.”

Amesema wateule hao kila mmoja ametimiza wajibu wake, na wengi wana sifa zao, hata kwa wale ambao wameteuliwa wanaotokea wilaya moja (Ileje) alipata ungumu lakini kwa utendaji kazi wao umewabeba.

JPM aagiza kura mchujo wa wagombea zihesabiwe hadharani
Morrison: Naogopa kupigwa