Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amehaidi kuufanyia kazi mchakato wa kura ya maoni kuelekea upatikanaji wa katiba mpya na kuendelea nao hapo ulipofikia kwani ni kwa faida ya watanzania wote.

Rais Magufuli ameyesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam alipokuwa akikabidhiwa Taarifa ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva.

Aidha amesema kuwa kazi imefanyika kubwa na Serikali ya awamu ya nne na mchakato umefikia sehemu nzuri,hivyo Serikali ya awamu ya Tano wataendelea hapo ulipofikia pale utakapofikishwa Serikalini kwani lengo ni kuipeleka Tanzania mahali pazuri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Mhe.Damian Lubuva amesema kuwa ucheleweshaji wa kura ya maoni umetokana na muingiliano na ratiba ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana na hivyo kushindikana kufanyika.

Pia amesema kuwa kwa sasa Tume ya Taifa ya uchaguzi itashirikiana na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ili kupeleka mapendekezo Serikalini ili kuangalia sehemu zinazoitaji marekebisho ili yafanyike na kukadhia kuwa hakuna kilichobadilika zaidi ya muda tu.

Mwenyekiti huyo ameongeza kuwa Tume imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha Daftari la wapiga Kura na kwa sasa hawatakuwa wakiandikisha wapiga kura kila baada ya miaka mitano kwani njia ya Biometric Voters Registration(BVR) kwa mwaka jana walifanikiwa kuandikisha wapiga kura milioni 23,161,440 sawa na asilimia 96.9 ambapo kanzi data hii itatumika kwa chaguzi zijazo na kurahisisha kuondoa waliopoteza sifa na waliosajiliwa zaidi ya mara moja na hivyo kufanya daftari hili kuwa la uhakika na la kuaminika.

Kukamilika kwa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kunakamilisha mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kuashiria kuanza kwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020 ambao rais ameagiza uanze mara moja

Mwanasiasa 'atingishwa' baada ya kujinadi kwa kula nyama ya Simba, twiga
Diamond Platinumz kuwa ‘mgeni Muhimu’ ndani ya E! Entertainment