Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameagiza wakulima wote nchini kuacha kuuza mazo kwa bei ya chini hasa kwa mwaka huu baada ya Dunia kukubwa na Corona kwani baadae kutakuwa na uhitaji mkubwa wa chakula na watauza kwa faida.

Ametoa agizo hilo leo Mei 30, Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi katika eneo hilo iliyoshuhudiwa na marais wastaafu pamoja na mke wa hayati Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere.

Rais Magufuli amesema amebaini kuwa tayari kuna wafanyabiashara ambao wameanza kununua kwa wingi mazao kwa bei ya chini kwa wakulima jambo ambalo ni hatari kwani kutakuwa na uhitaji mkubwa baadaye.

” Niwaombe wananchi na wakulima, inawezekana mwaka huu aua unaokuja usiwe mzuri sana, msiuze mazo yenu kwa bei za kutupa, baadae mtanunua hivyo vyakula kwa bei ya juu wakati njaa zitakavyo ingia”

” Tunafahamu maeneo mengi katika Afrika na katika Dunia yatapata shida ya chakula, ni kwasababu wali ‘jilock down’ wakati sisi tunalima…na kama tunaamua kuuza tuuze kwa bei ya juu sana, watwangeni kwelikweli”.

Aidha amesisitiza kuwa ili kupata faida ya nguvu ya mkulima licha ya kuuza kwa bei ya juu, wahakikishe wanauza mazao kwa muda muafaka.

Kisa cha Msukuma kufukuzwa Ikulu na Magufuli kwa kushindwa kutunza Tausi enzi za JK
Habari picha: Rais Magufuli akikabidhi Tausi kwa marais wastaafu, Maria Nyerere