Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli tayari amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.

Magufuli ametoa tamko hilo na kuwataka viongozi wa umma kuhakiki rasilimali na madeni yao kwa mujibu wa kifungu cha 9 na cha 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995.

Ambapo Jaji Nsekela amewaambia viongozi kuwa kufanya hivyo sio ombi bali ni kufuata katiba na sheria inazoziongoza nchi.

“Viongozi hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo na kuna sababu zake za msingi” amesema Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela.
Magufuli amemtaka Jaji Nsekela mwisho wa kupokea fomu hizo ni  tarehe 31 Disemba, 2017 kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha mpaka tarehe hiyo.

“Mhe. Jaji Nsekela ikifika tarehe 31 Desemba, ambayo ni siku ya mwisho kwa Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” amesisistiza Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki sambamba na tamko hilo, na amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine
 

 

Kenya yafuata nyayo za Tanzania
Video: Mbowe ahofia uchochezi, Siri ya Dk. Kimei kung'oka CRDB