Jeshi la Polisi Mkoani Pwani, limewakamata watu wawili wanaodaiwa kusafirisha bangi gunia 17 ndani ya gari lao lenye namba za usajili T. 819 CYQ aina ya Prado.
 
Kamanda wa polisi mkoani humo (ACP), Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo amesema kuwa, majina ya watuhumiwa hao yanahifadhiwa.
 
Amesema kuwa walipokea taarifa hizo kwamba watu hao walikuwa wanasafirisha shehena hiyo ya bangi wakipitia barabara ya Bagamoyo kuelekea Dar es salaam.
 
Aidha, Kamanda Nyigesa ametoa onyo, kwa wale wanaofanya biashara hiyo, wanaotumia na kusafirisha kuacha mara moja kwani inasababisha athari kwa afya na kuharibu vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
 
“Kama nilivyotangulia kusema kwa siku za hivi karibuni, hakuna mhalifu ama wahalifu watakaofurukuta mkoani hapa, kila atakayebainika atakutana na operesheni TINDUA TINDUA ya uhalifu, hivyo ni vyema wakaacha uhalifu, kusafirisha kwa magendo,”amesema Kamanda Nyigesa
 
  • Meya wa Iringa adaiwa kukamatwa akipokea rushwa
 
  • Polisi wahukumiwa kifo kwa kumuua mlinzi wa Mbunge

 

  • Video: Mawaziri vinara wa utoro Bungeni, Korosho kutoka Msumbiji zakamatwa Mtwara
 
Hata hivyo, Kamanda Nyigesa ameiomba jamii, wawatume popote na wamuite kokote na wakati wowote yeye ataitika, na wasisite kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu
Diwani wa Chadema afikishwa Mahakamani
Meya wa Iringa adaiwa kukamatwa akipokea rushwa

Comments

comments