Uongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesitisha mahafali ya wanafunzi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika leo mchana chuoni hapo jijini Dar es Salaam, ambapo Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alikuwa amealikwa na wanafunzi kama mgeni rasmi.

Tangazo lililobandikwa chuoni hapo na kushuhudiwa na wanahabari likiwa linamnukuu Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Apollinary Kamuhabwa limewakataza wanafunzi hao kutoweka mikusanyiko ya aina yoyote chuoni hapo.

Profesa Kamuhabwa kupitia tangazo hilo amewaonya wanafunzi hao kutojihusisha na masuala ya siasa wawapo chuoni kama ilivyo kwa watumishi wa umma.

Jitihada za waandishi wa habari kuzungumza na uongozi wa chuo hicho ili kupata ufafanuzi ziligonga mwamba baada ya kuelezwa kuwa hawakualika mkutano na waandishi wa habari.

UVCCM wamuamkia Lowassa kuhusu 'Siri za CCM'
Majani auona mwanga wa muziki wa Tanzania kwenye charts za Billboard