Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana ilisitisha Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupokea pingamizi dhidi ya mchakato wa uchaguzi huo.

Mahakama hiyo imewataka viongozi wa TFF, Mwenyekiti wa Uchaguzi na Bodi ya Wadhamini ya TFF na Rais wa TFF, Wallace Karia kufika mahakamani hapo leo, Julai 3, 2021 saa 3 asubuhi kujibu hoja dhidi yao.

Mchakato wa uchaguzi huo uliofanyika hivi karibuni, ulishuhudia wagombea wote wakiondolewa kwenye mchakato kwa kukosa vigezo, hatua iliyosababisha Rais wa sasa wa TFF kubaki kama mgombea pekee.

Baadhi ya wagombea walionesha kulalamika wazi wakidai kuwa kulikuwa na mchezo usio halali kwenye Kamati ya Uchaguzi. Madai mengine ni kuwa vigezo vilivyowekwa vilikuwa vigumu vinavyompa nafasi zaidi Bw. Karia.

Chadema wakaidi agizo la Rais Samia, wadai ‘hawatapiga goti’
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 2, 2021