Mahakama ya katiba nchini Gabon imethibitisha kuwa Ali Bongo ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Agosti 27 nchini humo.

Rais Bongo alipata 50,66% na mpinzani wake ambaye alikuwa mwenyekiti wa zamani wa Muungano wa Afrika Jean Ping  kupata 47,24%.matokeo ya awali yalionyesha ushindi wa bongo kuwa na tofauti ndogo ya kura.

Kwa mujibu wa matokeo ya mwisho yaliyotolewa na mahakama ya katiba Bongo alishinda kwa kura nyingi zaidi kutokana na kutobatilisha kura zilizopigwa katika ngome ya kiongozi huyo Haut-Ogoue.

Hatahivyo kura katika vituo 21 mjini Libreville vilifutwa kutokana na ombi la upande wa rais bongo ndio sababu kubwa ya kiongozi huyo kupata asilimia kubwa zaidi katika matokeo ya mwisho

Upinzani uliwasilisha malalamiko kupinga matokeo ya awali ya uchaguzi na kuiomba mahakama iamuru kuhesabiwa  upya kwa kura hizo, katika eneo hilo la Haut-Ogoue, magharibi mwa Gabon ambapo rais Bongo ndiyo ngome yake.

Serikali nchini Uganda Yapiga Marufuku Mapenzi ya Jinsia Moja
Taifa Stars Kujipima Na Ethiopia