Jaji wa mahakama Kuu nchini Kenya, Roseline Aburili ameagiza wakili wa upande wa upinzani, Miguna Miguna kuachiliwa kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Miguna Miguna alijaribu kurejea Kenya Jumatatu lakini akazuiwa kuingia baada ya kudaiwa kutowasilisha pasipoti ya Canada ambayo ilitumiwa kumsafirisha kwa nguvu hadi Canada.

Aidha, Wakili huyo wa upinzani aliwasili jana jumatatu akitokea nchini Canada na kuzuiliwa katika uwanja huo usiku kucha akitakiwa arudi nchini Canada.

Hata hivyo, Maafisa walijaribu kumsafirisha kutoka uwanja huo kwa kutumia ndege ya shirika la Emirates ambayo ilikuwa inaelekea Canada kupitia Dubai.

Serikali kugharamia mazishi kijana aliyefariki Mbeya
Nkurunzinza amtuhumu tena Kagame kuhusu jaribio la kumpindua

Comments

comments