Zikiwa zimebakia siku chache kufanyika kwa uchaguzi nchini Kenya, Mahakama nchini humo imetoa maamuzi kuwa matokeo yote ya kura yatatangazwa na wasimamizi wa vituo katika viwanja vya bunge.

Aidha, uamuzi huo umekuja mara baada ya jopo la majaji watano kusema kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi IEBC Nchini humo hana mamlaka kisheria ya kuhakiki na kutangaza matokea ya uchaguzi mkuu.

Kwa upande wa msimamo wa tume hiyo umeema kuwa ni lazima maafisa wake wahakiki matokeo yote kutoka katika viwanja vya bunge katika kituo kikubwa cha taifa cha kuhesabu kura na kwamba wana uwezo wa kubadilisha matokeo hayo.

Hata hivyo, uchaguzi nchini Kenya unatarajiwa kufanyika Agosti 8, 2017 pia unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta na mpinzani wake mkuu kutoka muungano wa NASA, Raila Odinga.

Video: Hivi ndivyo lilivyojipanga jeshi la polisi Dar katika sikukuu ya Idd El Fitri
Serikali yakanusha takwimu zilizotolewa na Gazeti moja hapa nchini