Mahakama ya Mkoa Vuga Zanzibar imeahirisha kesi ya ulawiti na udhalilishaji wa kijinsia inayomkabili Hassan Aboud Talib maarufu Kiringo hadi Machi 23, mwaka huu.

Hakimu Valestine Andrew Katema amesema kutokana na mahakama hiyo kuzuia  ombi la dhamana ya mshtakiwa, Wakili wa Upande wa mshtakiwa amepeleka ombi la dhamana katika Mahakama Kuu ili mshatakiwa huyo aweze kuwa nje wakati kesi ikiendelea kusikilizwa.

Mtuhumiwa huyo anashtakiwa kwa kumlawiti mtoto wa miaka 13, ambapo kwa mara ya kwanza ilisikilizwa Februari 26 na 27 anashtakiwa kwa makosa mawili la kwanza ni la kulawiti na la pili ni la kumtorosha mtoto huyo na kwamba itarudishwa tena mahakamani hapo baada ya mahakama Kuu kutoa uamuzi wake.

Mganga wa kienyeji mbaroni kwa kumpa bintiye ujauzito
Tshishimbi awapiku Okwi, Buswita

Comments

comments