Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mbonje amethibitisha kuwa jumamosi, Mei 12, 2018 msanii wa maigizo nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu aliachiwa huru na Mahakama kuu ya Tanzania mara baada ya kubadilishiwa kifungo na kutumikia kifungo cha nje.

“Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huru, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo chake nje, kitaalamu tunaita ‘community service’” amesema Mboje.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba 13 mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

 

 

Dkt Slaa afunguka kuhusu sakata la sh. 1.5 trilioni, "wanafanya ushabiki"
Namna ya kutibu ngozi kavu