Bundi linaendelea kutembelea maisha ya Mfalme wa RnB, R. Kelly ambaye hivi sasa anaandamwa na kesi za kuwanyanyasa kingono wasichana wadogo pamoja na madeni lukuki yakiwemo madai ya matunzo ya watoto.

Jana, mwanasheria wake alilazimika kuieleza Mahakama hali halisi ya uwezo wa kifedha wa mteja wake, kiasi cha kwamba amekuwa akiwapigia simu marafiki zake wamsaidie hata fedha ya kulipia dhamana.

Ingawa R Kelly alisaidiwa pia na rafiki yake kulipa deni la matunzo ya watoto kiasi cha $160,000, alishtakiwa pia na mwenye nyumba wake akimdai pesa ya kodi ya studio yake kiasi cha $200,000, mwenye nyumba huyo alishinda kesi na mahakama ikaamuru R.Kelly amlipe $173,000.

Aidha, kutokana na hali hiyo, nyaraka za mahakama zimeonesha kuwa akaunti kadhaa za R.Kelly zimekauka, nyingine ikiwa na salio la chini ya $13, lakini kwa muunganiko wa akaunti zake mbili ana salio la $625 pekee.

Pamoja na hali hiyo, mwenye nyumba wake bado anamdai $50,000. Complex imeripoti kuwa wadeni wake wamejaribu kutafuta lebo ya muziki ya Sony kuona kama wanaweza kupata salio la R.Kelly, ingawa lebo hiyo imeweka wazi kuwa hivi sasa haidaiwi chochote na mwimbaji huyo. Sony walikama mahusiano na mwimbaji huyo tangu Januari mwaka huu.

Serikali yatoa masharti kwa wanunuzi wa viwanja Dar, yaonya
Paris: Moto wateketeza kanisa la kihistoria ‘Notre-Dame’

Comments

comments