Mahakama Kuu nchini Kenya imekitangaza kifungu cha sheria ya Habari na Mawasiliano ya nchi hiyo kinachounda kosa la ‘matumizi mabaya ya mtandao na vifaa vya mawasiliano, kuwa ni haramu na kiko kinyume cha Katiba.

Jaji wa Mahakama Kuu nchini humo, Mumbi Ngugi alitangaza uamuzi huo jana, akikitaja kifungu cha 29 cha sheria hiyo kuwa kibovu na kinavunja sehemu ya Katiba ya nchi hiyo.

Ingawa Mkurugenzi wa  Mashtaka ya Umma (DPP) na Mwanasheria Mkuu wa nchi hiyo walikitetea kifungu hicho kwa madai kuwa kililenga katika kulinda heshima ya watu wengine ili wasichafuliwe au kukashfiwa kwenye mitandao, Jaji Ngugi alisisitiza msimamo wake na kueleza kuwa kama mtu atachafuliwa jina lake (defamed) atatumia vifungu vingine vya sheria zilizopo zinazotoa nafasi hiyo.

“Kama nia ilikuwa kulinda heshima ya watu wengine wasikashfiwe, basi kuna vifungu vingine vya wazi kwenye sheria ya Kashfa,” alisema Jaji Ngugi.

Uamuzi wa Jaji Ngugi ulipokewa kwa furaha na watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii nchini humo na kuzua gumzo zaidi kwenye mitandao ya kijami hususan mtandao wa Twitter.

Jerry Muro: Leo Tutalipiza kisasi cha Kipigo cha Azam FC Tunisia
Zitto Kabwe amvaa Waziri Kitwanga, asema sio saizi yake, ajipima na Rais Magufuli