Mahakama Kuu ya Uingereza, imetoa kibali kwa kundi la waomba hifadhi kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa mpango wa Uingereza kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda kuwa ni wa halali.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uingereza, imesema itatetea sera yake ambayo ni sehemu kuu ya mpango wa Waziri Mkuu, Rishi Sunak kukabiliana na idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili kwa boti ndogo.

Serikali ya Uingereza inasema mpango huo utazuia usafirishaji haramu wa binadamu. Picha ya REUTERS.

Hata hivyo, Serikali ya nchi hiyo inasema mpango huo utazuia usafirishaji haramu wa binadamu, ingawa umelaaniwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu tangu ulipotangazwa.

Aidha, safari ya kwanza ya ndege iliyopangwa kuwahamishia wahamiaji hao hadi Rwanda, ilizuiliwa mwezi Juni mwaka jana (2022), baada ya uamuzi wa dakika za mwisho wa Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu, ambayo iliweka amri ya kuzuia uhamishaji wowote hadi kukamilika kwa hatua za kisheria.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 18, 2023
Makamu wa Rais ziarani Mkoani Shinyanga