Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya kufanya mkusanyiko na kutotii amri halali katika geti la gereza la Segerea inayowakabili watu 27 akiwemo Halima Mdee na wabunge wenzake wawili.

Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuleta mashahidi mbele ya Hakimu Huruma Shaidi kwa ajili ya usikilizaji wa kesi hiyo.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Mei 5, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya ushahidi.

Saa chache kabla ya tamko la Facebook, Trump aanzisha tovuti yake
Mumbere aipeleka Simba SC nusu fainali 'CAF'