Mahakama Kuu ya Mtwara imeondoa Mahakamani shauri la kupinga matumizi ya kanuni za maudhui ya kimtandao( Online Content Regulation) lililofunguliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na wenzake dhidi ya Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Wengine waliofungua shauri hilo, ni Tanzania Human Rights Defenders (THRD), Baraza la Habari Tanzania (MCT), na Jamii Media, Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Jukwaa la Wahariri (TEF).

Kanuni hizo zilipaswa kuanza kutumika kuanza Mei 5 mwaka huu lakini mahakama ikaweka zuio baada ya kuwasilishwa kwa shauri hilo la kupinga mahakamani hapo.

Aidha, kesi hiyo namba 12/2018 ilisomwa mbele Jaji Mfawidhi, Dkt. Fauz Twaib na ilipangwa kutolewa maamuzi juu ya mapingamizi matatu.

Jaji Dkt. Twaibu amesema kuwa mahakama hiyo imekubali pingamizi moja kati ya matatu yaliyowasilishwa na taasisi hizo.

Hata hivyo, Mahakama imeondoa shauri hilo na kutoa nafasi kwa taasisi hizo kufungua shauri jingine kama zitakuwa hazijarizika na uamuzi huo.

 

Video: Mbowe alia siasa mazishi ya Bilago, Dk. Bashiru arithi mikoba ya Kinana.
Diogo Dalot anukia Old Trafford