Mahakama ya Wilaya ya Arusha imemhukumu kifungo cha nje Mkuu wa Chuo cha Uhasibu cha Arusha (IAA), Profesa Johannes Monyo baada ya kumkuta na hatia ya kuwapa ajira za kudumu wafanyakazi nane wenye elimu ya darasa la saba, kinyume cha sheria.

Akisoma hukumu dhidi ya Profesa Monyo, Hakimu wa Mahakama hiyo, Devotha Msofe alisema kuwa mahakama imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja, baada ya kujiridhisha pasipo shaka kuwa alitumia vibaya madaraka yake kuajiri watumishi hao nane.

Hakimu Devota alisema kuwa Profesa Monyo aliwapa ajira za kudumu wafanyakazi hao wenye elimu ya darasa la saba bila kupata kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi au Katibu Mkuu Utumishi, kinyume cha sheria ya utumishi wa umma.

Alieleza kuwa kifungo hicho cha nje kimetolewa kwa masharti ya kutofanya kosa lolote ndani ya kipindi cha mwaka mmoja akiwa anatumikia kifungo.

Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Adam Kilongozi awali aliiambia Mahakama hiyo kuwa Profesa Monyo alifanya kosa hilo Juni 2010. Aliwataja waliopewa ajira hiyo kuwa ni Pamela Maboko, Samson Mbarya, Mawazo Ndaro, Juma Nyarutu, Lilian Ngowi, Godfrey Mollel, Musa Maiki na Salim Shaban.

Familia Ya Haji Mwinyi Ngwali Kulishtaki Gazeti Mahakamani
Leicester City Mabingwa Wa EPL 2015-16